Bukobawadau

MBUNGE AZZA HAMAD ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VITUO VINNE VYA AFYA KISHAPU SHINYANGA

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad Jumamosi Mei 6,2017 amekabidhi Vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12.6 katika vituo vya afya vinne vya afya ambavyo ni Nhobola,Songwa,Ng’wang’haranga na Dulisi vilivyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga 
Vifaa tiba hivyo ni Vitanda sita vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama wajawazito,vitanda sita kwa ajili ya kulalia wagonjwa,shuka 12 na viti sita kwa ajili ya wagonjwa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alisema vimetolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania na vitasaidia katika kupunguza adha wanayopata akina mama wajawazito wanapofika kupata huduma katika vituo vya afya.
“Akina mama ndiyo wanapata adha kubwa wanapohitaji huduma za afya,baada ya kuona jinsi akina mama hawa wanavyoteseka,niliamua kuanza kutafuta watu wa kutusaidia,nashukuru ubalozi wa China nchini ulikubali kunipatia vifaa hivi kwa ajili ya wananchi wa Shinyanga”,alieleza Hamad.
“Vifaa hivi vitasaidia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto,naomba mvitunze”,aliongeza Hamad.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuachana na tabia ya kuozesha watoto wadogo kwa tamaa ya mali ‘ng’ombe’ kwani takwimu zinaonesha kuwa watoto wanapopata ujauzito inasababisha wengi wao kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
“Mkoa wa Shinyanga tunaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni,naomba tupeleke watoto shule,waacheni watoto wa kike wasome,wakifeli darasa la saba watafutieni shughuli ya kufanya siyo kuwaozesha,ni hatari kwa maisha yao”,aliongeza Hamad.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kuzitaja baadhi ya changamoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali wilayani kuwa ni upungufu wa watumishi,magari ya wagonjwa na miundo mbinu. 
Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio wakati mbunge Azza Hilal Hamad akiwa wilayani Kishapu kukabidhi vifaa tiba pamoja na kuzungumza na wananchi

Hapa ni ndani ya kituo cha afya Nhobola wilayani Kishapu-Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo ya Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola kilichopo kata ya Talaga,Bhujiku Mganga Nyanda
Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola Bhujiku Mganga Nyanda akieleza jinsi akina mama wajawazito walivyokuwa wanapata changamoto wakati wa kupata matibabu
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika wodi ya wazazi amebeba mtoto wa mkazi wa Kata ya Talaga baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha Nhobola
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akifurahia kubeba mtoto mwingine aliyezaliwa katika kituo cha afya Nhobola Mwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF) akimkaribisha Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) katika mkutano wa kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Nhobola
Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Hellena Chacha akizungumza katika kituo cha afya Nhobola kabla mbunge Azza Hamad kuendesha zoezi la kukabidhi vifaa tiba 
Kaimu katibu Umoja wa Akina mama wa CCM mkoa wa Shinyanga Rhoda John akizungumza katika kituo cha afya Nhobola
Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu akielezea changamoto zilizopo katika vituo vya afya,zahanati na hospitali wilayani Kishapu
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF) akifungua mkutano wa mbunge Azza Hilal Hamad katika kituo cha afya Nhobola
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF) 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea kuhusu msaada wa vitanda vya kujifungulia,kulalia na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Nhobola
Vitanda vitatu vya kulalia wagonjwa,kitanda kimoja cha kujifungulia na viti vya wagonjwa vilivyotolewa katika kituo cha afya Nhobola
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha kitanda cha kisasa cha kujifungulia
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha kitanda cha kulalia wagonjwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shuka zitakazotumika katika vitanda alivyopeleka katika kituo cha afya Nhobola
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi kitanda cha kujifungulia kwa viongozi wa kijiji,kata na wilaya ya Kishapu
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa kata ya Talaga
Diwani wa kata ya Talaga Richard Kazangu Dominiko( CCM) akitoa neno la shukrani baada ya mbunge Azza Hilal Hamad kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Nhobola
Mkazi wa kijiji cha Nhobola aliyejulikana kwa jina la Ng'wani Sali akimshukuru mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kupeleka vitanda katika kituo cha afya Nhobola 
Hapa ni katika kata ya Songwa-Pichani wakazi wa kata ya Songwa wilayani Kishapu wakijiandaa kumpokea Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)  alipowasili katika kata ya Songwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda,shuka na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Songwa
Wananchi waliobeba matawi ya miti wakiwa wamemzingira Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) alipowasili katika kata ya Songwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda,shuka na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Songwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amefungwa nguo huku akiandamana na wananchi kuelekea eneo la mkutano wa hadhara katika kata ya Songwa
Wananchi waliobeba matawi ya miti wakiandamana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
Maandamano kuelekea eneo la mkutano yakiendelea
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akifurahia na wananchi waliompokea
Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza baada ya mgeni rasmi mheshimiwa Azza Hilal Hamad kufika eneo la mkutano kabla ya kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Songwa 
Wacheza ngoma wakisalimiana na Mbunge Azza Hilal Hamad (CCM)
Wacheza ngoma ya asili 'Wanunguli' wakitoa burudani
Mcheza ngoma ya Ununguli akimshika nyoka
Mcheza ngoma ya Ununguli akiwa amemkamata nyoka
Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Hellena Chacha akiwasalimia wananchi wa kata ya Songwa
Diwani wa kata ya Songwa Abdul Mohammed Ngolomole akiteta jambo la mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Kwaya ya AICT ikiimba wimbo wa amani
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza wakati kwaya ya AICT ikiimba wimbo wa amani ambao ulimfurahisha na kuwaahidi kuwadhamini ili waurekodi wimbo huo
Akina mama wakiimba shairi
Diwani wa kata ya Songwa Abdul Mohammed Ngolomole akizungumza wakati wa mkutano wa mbunge Azza Hilal
Suzana Yohana akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa kata ya Songwa 
Mzee Hamis Bulege akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge Azza Hilal Hamad,zawadi iliyotolewa na wazee wa Songwa ikiwa ni ishara ya kuwa wanamkubali kama kiongozi mzuri anayejali wananchi wake
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akipokea zawadi ya mbuzi
Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu akizungumza
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wananchi wa kata ya Songwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizunguza
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akisitiza jambo
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vitanda vya kulalia na kitanda cha kujifungulia pamoja na viti vya wagonjwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akionesha shuka zilizotolewa katika kituo cha afya Songwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza baada ya kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Songwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau