Bukobawadau

WAZIRI WA KLIMO MIFUGO NA UVUVI, MH. CHARLES TIZEBA TAYARI AMEWASILI MANISPAA YA BUKOBA KATIKA KILELE CHA WIKI YA MAZIWA KITAIFA.

Mh. Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh. Charles Tizeba, akisalimiana na Msajili wa Bodi ya Maziwa, Bwn. Nelsoni Kilongozi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera mapema leo
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Tayari amewasili Mkoani Kagera katika Kilele cha Wiki ya Maziwa, Maadhimisho ambayo yamekuwa yakiendelea Takribani wiki nzima sasa, katika Manispaa ya Bukoba katika viwanja vya Kyakairabwa.
Maadhimisho haya yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kagera, Yanafanyika kwa mara ya 20 sasa ikiwa ni mfulululizo tangu kuanzishwa kwa wiki hii ya maziwa Kitaifa nchini, chini ya Usimamizi wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), ambao ndio waandaaji.
mara baada ya kuwasili uwanja ndege na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh, Deodatus Kinawiro, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, msafara umeelekea Viwanjani Kyakairabwa ambapo huko ndipo shughuli inapofanyika.
Waziri Tizeba, mara baada ya kuwasili viwanjani hapo, amepokea maandamano ya wadau wa maziwa wakiongozwa na wanafunzi pamoja na walimu wao kutoka shule mbalimbali za manispaa ya Bukoba, kisha kuanza kukagua na kutembelea mabanda mbalimbali.
 Sehemu ya wadau wa maziwa waliohudhuria viwanjani hapa wakiendelea kufuatailia moja ya burudani viwanjanai Kyakairabwa katika Kilele cha Wiki ya Maziwa
 Taswira ya Jukwaa kuu, wanaonekana Viongozi Mbalimbali wa Mkoa Kagera, Katikati Ni Mh. Waziri Tizeba, anaonekana anasaini Vitabu vya Washiriki wa maadhimisho haya ya 20 ya Wiki ya maziwa.
 Katika Banda la Halmashauri ya Bukoba wanaonekana Wadau na wawakilishi wa Idara, Ndg, Msabila Rafaeli na Method Kanyambo wakizidi kuweka uangalizi wa hali ya juu katika Banda lao, kuhakikisha wanafikia lengo la wiki hii.
 Pichani wanaonekana wanafunzi kutoka shule mbali mbali za Manispaa ya Bukoba, wakiwa tayari kumlaki Mh. Waziri Tizeba, Katika Viwanja Viwanaja vya Kyakairabwa.
 Pichani wanaonekana wanafunzi kutoka shule mbali mbali za Manispaa ya Bukoba, wakiwa tayari kumlaki Mh. Waziri Tizeba, Katika Viwanja Viwanaja vya Kyakairabwa.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wadau wa Maziwaya, Daktari Ally Majani akisoma Risala ya wadau wa maziwa mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri wa Kilimo Mifugo, na Uvuvi Charles Tizeba, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya maziwa Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kyakairabwa,  Bukoba Mkoani Kagera.
 mtoto Peace anaelelewa katika kituo cha Watoto yatima Cha NUSURU YATIMA -Kashai, akiadhimisha wiki ya Maziwa baada kujipatia pakiti yake.
 Wazee wanaohudumiwa katika Kituo cha MAKAO YA WZEE - KIILIMA, wakifurahia ladha ya Maziwa katika wiki ya Unywaji Maziwa, Kama Wanavyoonekana katika Picha. Kituo hiki chenye idadi ya Wazee 19, wakiume 12 na wa kike saba, kilianzishwa mwaka 1977.
 Wazee wanaohudumiwa katika Kituo cha MAKAO YA WZEE - KIILIMA, wakifurahia ladha ya Maziwa katika wiki ya Unywaji Maziwa, Kama Wanavyoonekana katika Picha. Kituo hiki chenye idadi ya Wazee 19, wakiume 12 na wa kike saba, kilianzishwa mwaka 1977.

Ni mtoto Davis Rwegasira kama alivyokutwa na camera yetu akiiadhimisha Wiki ya Unywaji maziwa, mapema leo Kituoni kwao Mugeza Mseto.

Zoezi la ugawaji Maziwa likiendelea chini ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Kinawiro, katika Kituo cha Kulelea Watoto yatima UYACHO - Hamugembe.
 Banda la TADB benki ya maendeleo ya kilimo, pichani ni Bwn. Saidi Mkabakuli
Next Post Previous Post
Bukobawadau