Bukobawadau

NAAM! WAMEPENDEZA NI MR & MRS GHALIB..!
Ni vema tukafahamu kwamba siri ya furaha ya kweli haipo katika vitu tulivyo navyo au vile tusivyo navyo, haipo katika vile vinavyotokea au visivyotokea kwetu, Kitu cha muhimu zaidi na ambacho kimekuwa chimbuko la furaha ya kweli ni uhakika na umadhubuti wa penzi au "upendo wa kweli". Wale waliobahatika kumpata mtu wa kushiriki maisha katika furaha hii, basi hao wanakubaliana na nasi jinsi ambavyo hii imekuwa ni zawadi njema kutoka kwa Mungu

Ni Shughuli ya Bwana Gharib Issac aliyoandaliwa na Mama yake mzazi iliyofanyika Juma lililopita katika Ukumbi wa Linas Night Cluba Bukoba.

Mwanzo wa matukio ya picha wakati wawili hao wakiingia ukumbini kwa miondoko mwanana kwa kucheza na kuamsha hoihoi nderemo

Gharib na Aidah wakikata utepe tayari kwa kuingia ukumbini

Bi Sharifa Karwani pichani akisama safi kabisa 'namna wawili hao walivyopendeza'

Mdau Juliano Mero akifurahi miondoko ya Bwana Gharib na Bobie Aidah wakati wakiingia ukumbini

Umati wa watu ukumbini

Naam!Wahaya wanasema 'Banula'!! Na kila mmoja alipenda namna wawili hawa walivyopendeza ni ndani ya ukumbi wa Linas Bukoba,tukio lililochukua kasi na kuwavutia watu wengi ni mwendo wa shangwe,Ndelemo ,Vikeleshendo 'nakaganja' hongera kwako Bi @aidahfaith na mmeo #gharib hongera pia @muky_da_hustler kwa shughuli ya dada yako ,hongera Mama Gharib na Da'Farida
Photo credit @bukobawadau 📸Kwa picha kali zenye kupendeza wasiliana nasi 0784505045 /0754505043


Wakiingia Ukumbini kwa kucheza Step nzuri na mavazi yaliyowapendeza vyema

Ujumbe wetu kwako bwana Gharib Issaac ;Wako wale wanaume ambao huwaumiza sana wapenzi wao na kuziumiza sana hisia za wapenzi hawa huku wakijitetea eti wanafanya hivyo kwasababu ya mapenzi, utaskia "It is because I care toomuch about you" let me tell you brother. Kama unamjali hautomuumiza yeye wala hisia zake tena kwa makusudi, stop excuses, usifiche tabia yako ya ufedhuli kwenye kivuli cha kujali au kupenda, tunaojali huwa tunazilinda hisia zao, tunaojali huwa tunaheshimu mawazo yao, tunaojali huwa tunawatiamoyo, tunaojali huwa tunaruhusu wao kujaribu mawazo yao, tunaojali huwa tunawaelekeza kwa upendo na sio kwa mabavu, tunaojali huwa tunajishusha pale tunapoona tumekosa na tunakubali makosa kiurahisi, tunaojali wala hatuko manipulative, tunaojali tukotayari wakati wote kuwa msaada kwao, by the way hata uwaamshe usiku wa manane wanajua fika kuwa tunawajali, muulize huyo wakwako usikilize jibu lake. Pamoja na kufanya hayayote kwao wala hatujawahi kujuta na wala haijapunguza nguvu zetu za kiume, kwanza on contrary mambo ndio yanazidi kuwa mazuri. Kama umesahau maana halisi ya neno kujali basi tafuta kamusi

Bi Aidah muda mchache kabla ya kuingia ukumbini tunachoweza kusema kwako ni ujumbe huu kutoka kwa Ndoa furaha ;Watu wengi walioko kwenye ndoa na mahusiano serious wakikueleza tofauti uliyopo kati ya vigezo walivyokua navyo awali vya wake au waume walokua wanawataka na walionao ndo utaelewa kuwa mapenzi ni kwa wale wanaoweza kuyaamsha ndani ya mtu. Na ndo utaelewa pia kuwa hisia za mapenzi huamshwa kwa uzuri wa ndani wa mtu na si kama wengi wanavyodhani.
Kwa ushauri zaidi wasiliana nao WhatsApp. 0622 786 707,Instagram. ndoa_furaha
Email. ndoafuraha@gmail.com

Tukio la kukata Keki

Bwana harusi na bibi harusi wakikata keki iliyokuwa imeandaliwa.

Hizi ni Swagar wakati wa kulishana Keki..


Mshangao !! ni wakati mshereheshaji akitoa maelezo kwa wawili hao kuhusiana na utaratibu wa Keki


Bwana Gharib Isaac na mwenzake Bi Aidah wakimlisha keki mmoja wa waalikwa ikiwa ni Ishara kwamba atakaye wahi basi hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa mtoto wa kwanza watakaejaliwa kumpata.

Baadhi ya waalikwa ukumbini wakifatilia mwanzo mwisho kila kinachoendelea

Bi Aidah akimkabidhi keki mama mkwe wake.

Pongezi za furaha kutoka kwa Bibi yake...

Kwa pamoja wakifungua Champagne katika sherehe yao


Waalikwa wakiendelea kufatilia kila kinachoendelea ukumbumbini

Kwa haraka haraka wadau wakaomba kupata picha nasi bila hiyana haki ikatendeka

Hakika watu ni wengi ndani ya Ukumbi wa Linas Night Club

Muda mchache kabla ya zoezi la kupokea zawadi kutoka kwa makundi mbalimbali

Shughuli ni watu,ndivyo mambo yanavyozidi kuchamka na kunoga ukumbini


Mashost wa Bi Aidah wakiendelea kuamsha Shangwe Ukumbini kwa miondoka ya kisasa


#BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043

Waalikwa waliohudhuria shughuli hii maarufu kama 'Mjuburo' kapu la Mama

Wanafamilia Wakiendelea kutoa zawadi kwa Bwana Gharib na Bi Aidah

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe hii akitoa neno

Muendelezo wa matukio ya picha ukumbini


Shukrani za kipekee kwake Bi Anna pichani kushoto kwa kushirikiana na familia katika kufanikisha shughuli hiyo, iliyochukua kasi na kuvunja mtandao kwa majuma mawili Sasa.

Zawadi kutoka kwa Bibi yake Bi Aidah

Ni Vigumu kwetu #bukobawadaumedia kukufikishia matukio yote, ila tunafanya kila tuwezalo kukupatia taswira kwa kiasi kikubwa

Bi Aidah akipata picha maalum na Bibi zake

Zawadi ya Mswala kutoka kwa shangake yake Bwana Gharib Issac

Furaha kubwa kwake Bwana Gharib wakati utaratibu wa kupokea zawadi ukiendelea

Ukumbi ni Linas Night Club, Picha na Bukobawadau cont:0754 505043 / -784 505045

Zawadi kemkem kutoka kwa Mama Mzazi wa Bwana Gharib

Muonekano wa baadhi ya zawadi
MUHIMU:Unafahamu kunamambo flani kwenye hizi ndoa zetu mtu utayaona kama madogo au yakawaida tena unaweza kuyachukulia poa kumbe ni bonge la signal mbaya. Hivi inakuwaje mtu ameoa au ameolewa lakini hakuna kokote tunakokuona umeketi, umesimama wala unatembea na mwenza wako? Misibani uko mwenyewe, kanisani uko mwenyewe? Kwenye starehe uko mwenyewe, mikutano yakifamilia au ukoo unakwenda mwenyewe, kwenye picha za mitandaoni uko mwenyewe au na watoto tu, party za marafiki uko pekeyako, kwenye maharusi na masendoff unaketi na marafiki zako mwenza wako kalala home na hata ukilazimika kwenda naye basi utatafuta rafiki zako uketi nao au uzunguke tu ukumbini ukiwa unakunywa kuliko ukae naye meza moja, mikutano ya shuleni kwa watoto wenu tunakuona mwenyewe na kwingineko kwingi uko peke yako. Hivi nyie mmeoana kuwa pamoja kitandani tu??? Maana hata huko nahisi uko mwenyewe!!!! Aisee hiyo ndoa yenu lazima iko kwenye wrong parking


Hiyo ni zawadi ya kabati lenye bonge la hadhi

Pichani ni wadau walioweza kutumia fursa kuwatangazia waalikwa uwepo wa Shughuli nyingine sawa na hihi kutoka kwenye familia zao,shughuli itakayolindima ndani ya Ukumbi wa Linas Night Club

Taswira ukumbini baadhi ya waalikwa
MUHIMU:Unafahamu kunamambo flani kwenye hizi ndoa zetu mtu utayaona kama madogo au yakawaida tena unaweza kuyachukulia poa kumbe ni bonge la signal mbaya. Hivi inakuwaje mtu ameoa au ameolewa lakini hakuna kokote tunakokuona umeketi, umesimama wala unatembea na mwenza wako? Misibani uko mwenyewe, kanisani uko mwenyewe? Kwenye starehe uko mwenyewe, mikutano yakifamilia au ukoo unakwenda mwenyewe, kwenye picha za mitandaoni uko mwenyewe au na watoto tu, party za marafiki uko pekeyako, kwenye maharusi na masendoff unaketi na marafiki zako mwenza wako kalala home na hata ukilazimika kwenda naye basi utatafuta rafiki zako uketi nao au uzunguke tu ukumbini ukiwa unakunywa kuliko ukae naye meza moja, mikutano ya shuleni kwa watoto wenu tunakuona mwenyewe na kwingineko kwingi uko peke yako. Hivi nyie mmeoana kuwa pamoja kitandani tu??? Maana hata huko nahisi uko mwenyewe!!!! Aisee hiyo ndoa yenu lazima iko kwenye wrong parking


Muendelezondo wa matukio ya zawadi kutoka kwa ndugu ,jamaa na marafiki


Baadhi ya zawadi zilizotolewa ukumbini hapo ikiwa ni pamoja na fedha taslimu


Tunaendelea na mtiririko mzima wa matukio na Bukobawadau media Contact :0784 505043/ 0754 505043


Matukio yote na Bukobawadau media Contact :0784 505043/ 0754 505043


Zawadi kutoka kwa Bibi


Zawadi zikiendelea kutoka makundi mbalimbali, hakika shughuli imebamba isivyo kawaida

'Embaga'..! Umati wa watu ukumbini..!

Ni furaha kubwa kwa wawili hawa kama inavyoonekana kupitia picha


Matukio na Bukobawadau media Contact :0784 505043/ 0754 505043


Gharib na Aidah tunachoweza kuwaeleza katika maisha yenu ya ndoa ; Fahamu kwamba kila unalolinena au kulitenda katika mahusiano yako kwa kujua au kwa kutokujua lina nafasi ya kuyajenga au kuyabomoa mahusiano hayo. Kuwa macho sana na maneno unayoyazungumza na matendo unayoyatendaKatika Utayari mama Gharib kupokea zawadi kitoka kwa wanae, na kufuatiwa na makumbi mbalimbali ya kina Mama

Zawadi maalum kutoka kwa Bi Anna ikitangazwa ukumbini

Muendelezo wa matukio ya picha ukumbini


Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu

Bi Sharifa Karwani akipata picha na watoto wake, yeye ni Mama Mdogo wa Bi Aidah.

Picha mbalimbali kwa wanafamilia kwa ajili ya kumbukumbu


Muendelezo wa matukio ya picha kwa ajili ya kumbukumbu

Wakuitwa Bi Rukia Kassim

Ni dhahili kabisa inaonyesha moyo ukimdunda kwa kasi, anaishiwa puzi Bi Aidah huku machozi machungu yakimtoka ni wakati wa tukio linalowzindua watu wengi wakati mshereheshaji akitoa maneno yenye mafunzo na ujumbe mzito kuhusiana na ndoa..

Ni wakati wa mafunzo yote ya kwenda kwa mume, machozi yakiendelea kumtoa Bi Aidah.

Kushoto ni Bi Anna Rafiki mkubwa wa Wawili hawa aliyeweza kujitoa kwa asilimia kubwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa bin Sawia..

Marafiki wa Bi Aidah wakipata picha ya kumbukumbu mara baada ya kutoa zawadi zao

Sehemu ya wadau walioshiriki kufanikisha shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Linas Night Club

Kuelekea mwishoni kabisa mwa Shughuli hii BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043

 Mwisho kabisa Sasa unaweza kupata habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka Play Store

 BOFYA HAPA BUKOBAWADAU APP
Next Post Previous Post
Bukobawadau