Bukobawadau

MRADI WA KIISLAMU KARAGWE

 Uhusiano mwema baina ya waumini wa dini ya Kiislamu katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na watu wa mataifa ya Kiarabu Mashariki ya mbali umewasaidia kuharakisha upatikanaji wa maendeleo ya huduma bora za kijamii.

Hayo ymebainishwa na Sheikh mkuu wa wilaya ya Karagwe Sheikh Nassibu Abdul bin Abdallah wakati akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la masheikh wa mkoa wa kagera wakiongozwana na sheikh wa mkoa wa kagera alhaji haruna Kichwabuta waliotembelea kata ya Bugene kuadhimisha mazazi ya Mtume SAW
Sheikh Nassibu amesema wafadhili wa kiislamu kutoka Mascat Oman pia wanajenga msikiti na tanki la maji katika kijiji cha Mukakorongo pamoja na madrasa ya kufundishia elimu ya dini kwa thamani ya Sh17 milioni za Kitanzania.
 Aidha amesema miradi mingine inayoendelea ni katika upanuzi wa msikiti na matanki ya maji katika kijiji cha Nyakaiga kata ya Bushangaro inayogharimuzaidi ya Sh20.8 milioni hivyo kupunguza changamoto ya maji kwa waumini wa kiisalamu na hata madhehebu mengine walio jirani na miradi hiyo
Amesema miradi inayoendelea kujengwa ni pamoja na ujenzi wa matanki ya maji Kakiro na chuo cha kiisalamu cha Kakiro yenye thamani ya Sh4.8 milioni na ujenzi wa msikiti pia madrasati Mukakorongo chini ya ufadhili wa FAHMY FURNITURE STAFF & FRIENDS CHARITY kwa thamani ya Sh13.6 milioni
Sheikh mkuu wa mkoa wa kagera Alhaji Haruna Kichwabuta amewataka viongozi wa kiislamu kujenga na kuimarisha umoja na msikamano baina yao na waumini wa madhehebu mbalimbali ya kidini badala ya kutengana na kusababisha malumbano kwa kukiuka misingi ya kiimani
Sheikh Kichwabuta amesema hayo jana wakati akikagua na kuzindua msikiti wa kijiji cha Murusimbi kata ya Bugene uliojengwa na wafadhili kutoka Mascat Oman uliogharimu Sh16.46 milioni na tanki la maji lenye ujazo wa lita1,700 
Pichani Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta alitoa vyeti maalum kwa waliofadhili ujenzi wa miradi ya kiislamu wilayani karagwe
 Pia baraza la masheikh wa mkoa walikagua viwanja vya BAKWATA ambavyo vinatakiwa kuendelezwa kwa kupata hati miliki na kuviendeleza kwa kuwekeza miradi ya kiuchumi Mukakorongo
Aliwahimiza waumini kuacha utengano wa kimadhehebu ya kiislamu yakiwemo ya kikristo bali watangulize utu au ubinadamu mbele za Mungu kwa kuzingatia mafundisho ya kiislamu yanayoelekeza kuwajali na kuwasaidia ndugu jamaa na marafiki wakiwemo majirani
“Mtume Mohammad SAW wakati analazimishwa kuhama kutoka makka kwenda Madina waliojua maadui zake na kumtafutia njia ya kupita mmojawapo hakuwa mwislamu na alimsaidia kuokoa maisha yake” Alisema Kichwabuta
Pia aliwasihi waumini na wananchi kwa ujumla kutunza miradi inayofadhiliwa na wahisani wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuunga juhudi zinazofanywa na serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii.
Wilaya hiyo inayo misikiti 65 yenye kukadiriwa kuwa na waumini zaidi ya 12,300 ambao hupatikana katika mitaa minne ya kiisalamu wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwa lengo la kuongeza mapato kujikwamua kiuchumi.
KARAGWE : Na Shaaban Nassibu Ndyamukama
@bukobawadau 
Next Post Previous Post
Bukobawadau