Bukobawadau

BALOZI KAMALA APOKEA ZAWADI KUTOKA KWA KINAMAMA WA KATA ISHUNJU-KIZIBA

 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akipokea zawadi kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya kinamama wa Katika Ishunju na kumpongeza kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya, Balozi Kamala anaendelea na ziara yake jimboni kwa kukutana na wananchi na kuyasikiliza na kutatua matatizo yao.
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akitoa ufafanuzi kuhusu Mradi mkubwa wa Maji kutoka ziwa victoria utakaopita Vijiji vya Kata Ishozi,Ishunju na Kanyigo.
Baadhi ya wananchi wakendelea kumsikiliza Mbunge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala katika mkutano wake wa Kata ya Ishunju tarafa Kiziba Wilaya Missenyi
Mh. Msafiri Diwani wa Kata ya Ishunju akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano wa Mbunge na kumshukuru kwa kutoa mifuko 150 ya cement kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Rwemondo na shule ya Msingi Ishunju,Mh. Msafiri ametumia fursa hiyo kuwashukuru wana Lugoyo Social Club na familia ya Yustas Kamugisha maarufu kama (Nshomile Family) kwa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Ishunju.
 Wananchi wakifuatilia mkutano huo kwa umakini
 Bi Hadija Saidi Shabani Mtendaji wa Kata ya Ishunju akisoma taarifa ya maendeleo ya Kata.
Mh.Diwani Msafiri akitolea jambo ufafanuzi
 Mkazi wa Ishunju akitoa hoja yake mbele ya Mbunge.
 Wananchi wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali zinazotolewa.
 Taswira mbalimbali wakati mkutano ukiendelea
 Bi Hadija Saidi Shabani Mtendaji wa Kata ya Ishunju akiendelea akitoa muendelezo wa ratiba katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Kamala.
Mwalimu Elberius Leopord mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Rwemondo akielezea baadhi ya changamoto zilizopo shuleni hapo.

Next Post Previous Post
Bukobawadau