Bukobawadau

MSHUMAA UMEZIMA GHAFLA R.I.P RUGE

#pumzikaruge #tutaonanabaadae
Kwa masikitiko na majonzi makubwa, muda wa saa mbili usiku baada ya kuona kwenye mitandao ya kijamii tukio hili la kusikitisha juu ya kifo cha Ruge binafsi sikuamini.
Nilipofuatilia zaidi nilithibitisha baadaye kuwa ni kweli hatunaye tena Ruge duniani hakika moyo ulikufa ganzi na kupigwa butwaa.
Si kwamba nalaumu kwa kifo Bali nasikitika kwa pengo lake aliloliacha kwenye ardhi hii ya Tanzania.
Ruge ni nani hasa?
Kwa hakika ni kijana Mwenye fikra wekevu na pevu juu ya kubadilisha vijana kutoka kusubiri ajira na kujitegemea kiuchumi.
Ni kijana asiyeishiwa maneno yenye hekima na yenye mchango chanya kwa jamii.
Ni kijana Mwenye mawazo mapana juu ya kujikwamua kutoka kwenye utegemezi na kutafuta fursa.
Ni kijana anayechukia uonevu, uvivu na watu wenye fikra mgando.
Amekuwa kiungo kati ya ajira tegemezi na kuibua fursa kwa vijana mbalimbali na kwa jamii kwa ujumla.
Kwa hakika wasanii na tasnia ya Sanaa wamepata pengo kubwa sana kwa kuondoka kwa kioo cha sanaa.
Ni mengi naweza kuandika lakini naishia kwa kusema kazi ya Mungu haina makosa. Nenda Ruge nenda tangulia nasi tupo njiani japokuwa umeondoka bado mapema lakini mbaya zaidi hakuna Mwenye kujua siku wala saa.
Watanzania tunakulilia na kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe pumziko la milele. Amen!*BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE*
.
.
_____________
#pumzikaruge #tutaonanabaadae
Next Post Previous Post
Bukobawadau