Bukobawadau

BALOZI KAMALA ATEMBELEA SHULE YA BUNAZI GREEN ACRESS

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi dk. Kamala ametembelea shule ya Bunazi Green Acress,shule ya Kingereza inayofanya vizuri Wilayani Mishenyi na mkoa wa Kagera inayolenga kuendeleza ujuzi na vipaji vya watoto vilevile kuwaandaa katika kutimiza ndoto zao za kuwa wataalam wa kesho katika nyanja mbalimbali.
 Wanafunzi wa darasa la tatu na la nne wa shule ya Bunazi Green Acress wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule na mgeni wao Mbunge Balozi dkt.Kamala aliyetembelea shule hiyo na kuahidi kutatua baadhi ya changamoto
Balozi dkt Kamala katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Bunazi Green Acress, Mh Kamala ameza kuzipokea changamoto zote zilizotolewa shuleni hapo pamoja na kuahidi vifaa vya michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo


Bi Tibanga ambaye ni Meneja wa Shule ya Bunazi Green Acress akiongoza msafara ulioambatana na Mbunge kukagua baadhi ya miundombinu ya shule hiyo.
 Baadhi ya watumishi wa Shule ya Kingereza ya Bunazi Green Acress
Muonekano wa Sehemu ya Majengo ya Shule ya Bunazi Green Acress iliyoanzishwa na Dr. Julian Rushaigo BUJUGO ambaye pia nduye muanzilishi wa Shule za Creen Acress zilizopo jijini Dar es Salaam
Afisa Mahusiano wa shule hiyo Respicius John akielezea changamoto ya sheria zilizopo kupata vibali katika kuwajiri walimu wa Kigeni,nakumuomba Mh.Mbunge Balozi dkt.Kamala kufikisha kilio chao Bungeni

Next Post Previous Post
Bukobawadau