Bukobawadau

HIFADHI YA BURIGI-CHATO SASA KUMEKUCHA NI BAADA YA MFALME WA PORI KUPOKELEWA NA FAMILIA YAKE KUTAWALA ENEO HILO

• Je Wajua Kuwa Nusu ya Simba Wote Duniani Wapo Tanzania?
Na: Sylvester Raphael
Burigi- Chato kumekucha sasa Mfalme wa Pori (Simba) na familia yake awasili katika hifadhi hiyo ya Taifa ili kutawala eneo hilo muhimu la utalii katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Ni ukoo mmoja wa simba 20 ukiwa na simba wazima 17 na simba watoto 3 wapokelewa katika lango la Nyungwe Hifadhi ya Taifa ya Brigi-Chato Februari 6, 2020 na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti.
Katika Simba hao 20 Baba anaitwa Brigi na mama anaitwa Chato wakiwa na familia yao ya simba wengine 18 waliwasili Nyungwe katika Hifadhi ya Burigi-Chato majira ya saa 5:00 asubuhi wakisafirishwa kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara na dhumuni la kuwaleta simba hao ni kuhakikisha hifadhi ya Burigi- Chato inakuwa na wanyamapori wote hasa wale wakubwa watano ili kuvutia zaidi utalii.
Kwaniaba ya wananchi wa Mkoa wa Kagera na Geita mara baada ya kuwapokea Simba hao 20 wakiongozwa na baba Burigi na Mama Chato Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa neno la kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuamua kuanzisha Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato katika ukanda wa Kaskazini Magharibi ili kufufu upya uchumi wa mikoa ya Kagera na Geita kupitia utalii.
“Sisi wananchi wa Kagera tunayo furaha sana kuwapokea Simba hawa kwani katika eneo hili uchumi wetu utakua kwa kasi, lakini nimshuru tena Mhe. Rais Magufuli kwa maamuzi yake sahihi kuanzisha hifadhi hii kumesaidia sana, hakuna asiyejua kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na hatari sana katika maeneo haya ya Burigi kwa majambazi kutumia hifadhi hii kuteka wananchi l pia kuendesha vitendo vya kiharamia lakini sasa hakuna tena.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwashukuru pia uongozi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kuamua Hifadhi ya Serengeti itoe Simba 20 ili waletwe katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato ambapo aliwahaidi yeye kwakushirikiana na wananchi wa mkoa wa Kagera watahakikisha kuwa hakutakuwepo na changamoto zozote zitakazojitokeza ambazo ziliwahi kujitokeza katika Hifadhi nyingine za Taifa.
Kamishina wa Uhifadhi Martin Loibooki ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Magharibi kwaniaba ya Kamishna Mkuu Dkt. Allan Kijazi akieleza sababu za kuhamisha simba 20 kutoka Serengeti kuja Burigi-Chato alisema kuwa katika hali ya kawaida kuna wanyama wanaokula nyasi na kuna wanayama kama simba wanakula nyama au wanakula wanyama wezao na hilo linasaidia katika ekolojia ya wanyamapori .
Kamishna Loibooki alisema pia katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato siyo mara ya kwanza hifadhi hiyo kuwa na Simba na ndiyo maana kuna maeneo katika hifadhi hiyo yanajulikana kwa jina la Mllima wa Simba lakini kutokana na shughuli za kibinadamu na uvamizi wa hifadhi hizo simba waliweza kutoweka kwa kuuawa na binadamu ili wasidhurike na ndiyo maana simba wakatoweka.
 Naye Dkt. Denis Itanda Mtafiti Mkuu wa wanyamapori aliyeongoza jopo la Madaktari na wataalam kuhakikisha simba 20 kwanza wanakamatwa kule Serngeti wananwekwa kwenye vitenga na kusafirishwa salama hadi katika Hifadhi ya Burigi-Chato alisema kuwa Tanzania ina (simba 15000 waliopo ndani ya mipaka ya Tanzania) nusu ya Simba wote duniani jambo ambalo ni la lakujivunia pia nchi ya pili kwa wingi wanyamapori duniani.
Dkt, Denisi alisema kuwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ndiyo hifadhi yenye Simba bora duniani na katika miaka mitano Simaba wameongezeka kwa kiwango kikubwa baada ya Serikali kuamua kupambana na ujangiri na uwindaji haramu katika hifadhi zote nchini na ndiyo maana Serikali imeamua kuhamisha Simba 20 kuja katika hifadhi za Burigi-Chato.
Simba hao 20 tayari wamewekewa vifaa maalum vya kuhakikisha kila mara walipo kama ni salama lakini pia vifaa hivyo vitasaidia kuwaongoza watalii kujua Simba hoa wapo wapi kwa siku husika ili wakawaone kirahisi. Dkt. Denisi anasema kuwa mara baada ya simba 20 kufikishwa eneo wanalotakiwa kuachiwa watawekwa kwenye uzio na kuwa chini ya uangalizi wa wataaalam kwa wiki mbili na baadae watakuwa wanaachiwa wachache wachache.
Kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. More Msua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori alimshukuru Mkuu wa Mkoa Kagera kukubali kuwapokea Simba hao pia alimhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha Wanyamapori wakubwa watao (The Big 5) wataletwa katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato ili kuhakikisha watalii wanapofika ktika hifadhi hiyo wanawaona wanyama hao wote.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Saada Malunde akishiriki katika zoezi la kupokea simba 20 alisema wananchi wa Biharamulo wapo tayari kuwalinda wanyamapori hao kwa kushirikiana na TANAPA ili Hifadhi ya Burigi-Chato iweze kushamiri. Hifadhi ya Burigi- Chato ina ukubwa wa kilometa za mraba 470.
Next Post Previous Post
Bukobawadau