Bukobawadau

MAZISHI YA MPENDWA WETU MA VICTORIA KABAKAKI MUHAZI KIJIJINI BUGANGUZI


Hivi ndivyo Mazishi ya mpendwa wetu Mama yetu Ma Victoria Muhazi yalivyokuwa..kupitia Bukobawadau pichani ni sehemu ya Wanafamilia wakishiriki Ibada ya Mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Kijijini Bugangazi na kuhudhuriwa na umati wa wananchi naViongozi mbali mbali wa vyama vya siasa, dini na serikali.
Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana akiwa ameungana na wanafamilia katika mazishi yaMpendwa wetu Bi Victoria Kabakabiki Muhazi,Mazishi yaliyoudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa serikali, vyama vya siasa na taasisi za umma

Umati wa waombolezi wakiendelea kushiriki Ibada hiyo.

Jeneza likiwa limebebwa ...kuelekea ukumbini kwa ajili ya Misa ya mazishi...Endelea kuwa nasi kwa mtiririko mzima wa matukio ya picha...


Neno la bwana likisomwa na mjukuu wa marehemu,Mtoto mkubwa wa Dada Magdalena Muhazi...


Mama Leonida Muhazi akiteta jambo na kijana wake Ibra Muhazi...
Wakipkea maelekezo kutoka kwa Kaka Andrew Muhazi...
Ibra Muhazi,Isack Muhazi na Mtaalam Andrew Muhazi wakiteta jambo...
Umati mkubwa wa waombolezaji wakiwa wamehudhulia Mazishi ya Mpendwa wetu Victoria Muhazi yaliyofanyika Nyumbani kwake kijijini Buganguzi siku ya Alhamisi Tarehe 18 June,2020.


Muendelezo wa matukio ya picha..

Padre akiongoza mazishi hayo...Anaitwa Aron Gozberth pichani kulia wakiendelea kushiriki Ibada ya mazishi ya shangazi yake ,Mpendwa Ma Victoria Muhazi.


Muendelezo wa matukio ya picha....

Muendelezo wa matukio ya picha, Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Ma Victoria MuhaziKuelekea kutoa heshima za mwisho...

Ndugu Mwambi Rwihula akitoa sadaka wakati wa tukio la kutoa heshima za mwigo kwa mpendwa wetu Ma Victoria Muhazi

Mama Leonida muhazi akiwa ameongozana na Vijana wake katika 'Last respect'

Zezozi la kutoa heshima za mwisho likiendelea..kwa waombolezaji wote...


Endelea kufuatilia kurasa zetu za Instagram na facebook kwa matukio zaidi ya picha.

Kaka Hermes Muhazi akitoa heshima zake za mwisho.

Simanzi kubwa Dada Anitha Muhazi na Dada Grolia Muhazi wakitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa Mama yao mzazi, Mpendwa Victoria Kabakaki Muhazi.
Dada Grolia Muhazi na Anitha Muhazi wakati wakitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa Mama yao mzazi, Mpendwa Victoria Kabakaki Muhazi.


Tangulia Mama yetu mpendwa Victoria Muhazi na sisi tunafuatia Pole sana ndugu wanafamilia....
Muendelezo wa matukio...

Wasifu wa Marehemu ukitolewa na Mtoto wake mkubwa Kaka Hermes Muhazi,lmest Muhazi...
Salaam za rambirambi kwa niaba yaWajukuu zikitolewa na Ms Collin Mahende.Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango akitoa salaam za rambirambi kwa familia ya mzee MuhaziMkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango akikabidhi rambirambi yake.Mh.Muganyizi Zachwa mwenyekiti wa CCM manispaa ya Bukoba,akitoa salaam za rambirambi

Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Bukoba, Muganyizi Zachwa akitoa salaam za rambirambi kama kiongozi na kama Mkwe wa familia ya Mzee Muhazi.


Wajomba wa familia hii, wakiendelea kufuatilia kinachojiri


Salaaam za rambirambi na mkono wa pole zikikendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali..

Ndugu wa marehemu Mama yetu Mpendwa,Kutoka Kishanda wakitoa salaam za rambirambi,

Salaam za rambirambi kutoka kwa Mama mkwe wa mpendwa wetu Stide R.I.P
Mama na Mtoto wa Marehemu Stide wakikabidhi ubani kwa familia....
Dada Masty Muhazi akipokea rambirambi...
Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu ,Ma Victoria Muhazi
Mwalimu Kashuku, pichani katikati akiwa ameungana na waombolezaji wengine, mazishi ya Ma Victoria Muhazi

Mtaalam Ibra Muhazi na rafiki yake Jimmy Apson marabaada ya mazishi ya mpendwa Bi Victoria Muhazi

Tutaonana badae mama yetu mpendwa....

Tangulia Mama yetu Victoria Muhazi nasi tunakuja,Hii safari yetu sote....


Tangulia Mama yetu mpendwa Victoria Muhazi na sisi tunafuatia Pole sana ndugu wanafamilia....
Tangulia Mama yetu mpendwa Victoria Muhazi na sisi tunafuatia Pole sana ndugu wanafamilia....

Umati mkubwa wa watu wakiendelea kushiriki mazishi ya mpendwa wetu Ma Victoria Kabakaki Muhazi

Eneo la kaburi ibada ikiwa inaendelea...
Eneo la ksburi mazishi ya mpendwa Ma Victoria Muhazi yakiendelea...

Utaratibu wa kuweka udongo kwenye kaburi ukiendelea....

Grolia Muhazi akiweka udongo kwenye kaburi la Mama yake mzazi.

Hakika ni simanzi na vilio ndivyo vimetawala kwa wanafamilia katika Mazishi ya Mama yao mpendwa ,Victoria Kabakaki Muhazi yaliofanyika nyumbani kwake kijijini Buganguzi
Mama neno tunaloweza sisi wanao nikuwa "tutakukumbuka Milele". Mama tulikupenda sana, lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi...

Waombolezaji wakiweka Udongo kwenye kaburi...
Mkuu wa Wilaya ya Muleba ,Mhandisi Richard Ruyango akiweka shada la maua
Collin Mahende Mjuu wa Marehemu akiweka shada la maua
Zoezi la kuweka mashada ya maua likiendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali


Grolia Muhazi,Anitha Muhazi na Frolida Muhazi kwa pamoja wakiweka shada la maua juu ya kaburi la baba yao mpendwa,Victoria Kabakaki Muhazi.
Michael Muhazi nawanafamilia,pole sana na msiba huu mzito.


Poleni sana wafiwa wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Ameen

Kaka Alex Muhazi akiweka Maua kwenye kaburi la Mama yake mpendwa,Victoria Muhazi


Kaka Vicent Peter Bushaija tunatambua sana uwepo wako


Katika hili na lile na Kaka Hermes Muhazi,Kada asiyetiliwa shaka huku akiamainiwa na makundi ya vijana
Tunapenda kutambua ushiriki wa familia ya Bushaija, familia ya Rwabizi sambamba kabisa na familia ya Rusenene.
Ms Aquilina Muhazi na Ndugu Peter Rushaki
 Anitha Muhazi  pichani
 Mama Leonida Muhazi akiteta na Mjukuu wake Ms Maxine Muhazi
 Issack Muhazi na Moses Muhazi wakicheck na Camera yetu...
Dokta Kamugisha Kamuzora,Gloria Muhazi,Andrew Muhazi na Jimmy Apson mara baada ya kumpimzisha mpendwa wetu Ma Victoria Muhazi
 
Picha za hapa na pale muda mchache mara baada ya mazishi ya mpendwa wao


Next Post Previous Post
Bukobawadau