Na: Sylvester Raphael
Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu imetia nanga
katika Bandari ya Bukoba leo Juni 28, 2020 majira ya saa 10 jioni
ikitokea mkoani Mwanza ikifanya safari yake ya kwanza mra baada ya
ukarabati kukamilika na kupokelewa na umati wa wananchi wa Mkoa wa
Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti
pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini.
Akiongea mara baada ya meli hiyo kuwasili Mkuu wa Mkoa Gaguti
alisema kuwa ni takribani miaka sita tangu MV Victoria isitishe safari
zake kutoka Bukoba kwenda Mwanza ambapo safari ya mwisho ilikuwa tarehe
18 Desemba 2014 na wakati huo Meli hiyo ikitegemewa na wananchi wa
Kagera kwa usafiri na usafirishaji wa mizigo ambapo tani moja ya ndizi
ilisafishwa kwa shilingi 27,000/=ukilinganisha sasa malori
yanasafirisha tani moja ya ndizi kwa gharama ya shilingi 100,000/= hadi
shilingi 120,000/=
Aidha, Mkuu wa Mkoa alisema kuwa Meli hiyo
sasa imeufungua tena mkoa wa Kagera kiuchumi kwa njia ya maji kuelekea
katika nchi za jirani za Uganda na Kenya. Pia alisema kuwa meli ya New
Victoria Hapa Kazi Tu ni mkombozi wa wananchi wote wa Kagera Bodaboda,
Mama lishe na wengineo sasa wamejipatia ajira rasmi.
Naye Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Bw. Humphrey
Polepole akiongea mara baada ya kuwasili ana meli hiyo alisema kuwa Meli
ya New Victoria Hapa Kazi Tu ipo vizuri na wataaalam wamethibitisha
kuwa hakuna hitirafu yoyote kwani imefungwa mitambo mipya ambayo ina
nguvu mara mbili ya ile ya awali iliyokuwemo jambo ambalo litapelekea
meli hiyo kufanya safari zake kutoka mwanza kuja Bukoba kwa saa sita tu.
Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu ina uwezo wa kupakia tani 200 za
mizigo na abiria 1200 aidha, imekarabatiwa kwa gharama ya shilingi
bilioni 22.8 na Kampuni ya JV of Gas Entec Company Limited, Kang Nam
Corporetion wakishirikiana na SUMA JKT. Pia Meli hiyo imefungwa mfumo
mpya wa kidigitali ambapo mfumo wote wa analojia uliondolewa.
Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu baada ya kutia nanga katika Bandari ya
Bukoba itaendelea kufanyiwa majaribio mbalimbali ya kitaalam ikiwa ni
pamoja na kwenda katika bandari ndogo ya Kemondo kabla ya kurejea Jijini
Mwanza na kubeba mizigo ya wanachi bule zaidi ya tani 100.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Jimbo Kuu la Bukoba, Dk Abelnego Mushahara
Sheikh Haruna kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera akitoa neno
Baba Askofu Desderius Rwoma,Askofu Mkuu Jimbo Katoliki Bukoba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment