Bukobawadau

#GERA UZINDUZI WA MAFUNZO MAALUM YA VIJANA YA KUJENGA UWEZO WA KUWEZA KUJIAJIRI


Viongozi wanaowania nafasi za uongozi wametakiwa kufanya maendeleo ambayo yataacha alama kwa vizazi vilivyopo na vijavyo na kuepukana na tabia za kuharibu miradi na miundombinu ya watangulizi wao
 Wito huo umetolewa na Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (MNEC) Kagera Ndugu Wilbroad pichani.
 Mh.Mtabuzi wakati akifungua mafunzo maalum ya vijana zaidi ya 200 yatakayotolewa kwa miezi mitatu katika kozi maalum kwa Vijana ya kujenga uwezo wa kuweza kujiajiri ;Elimu ya Ujasiriamali, Ujenzi, ufundi ushonaji ,umeme ,Ufugaji Nyuki ,Kompyuta na kilimo .
 Mh.Balozi Kamala akiteta jambo na Mh.Msafiri Nyme na Mh. William Osward Lutta

Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na Mbunge Balozi Dr.Deodurus Kamala yanalenga kuwafikia zaidi ya vijana 1,000 ambao hawakuweza kupata nafasi au Uwezo wa kuendelea na masomo baada ya kuhitimu Elimu ya msingi na Sekondari.
"Huu ni uongozi unaoacha alama,kama MTU atajifunzia fani Fulani atawafundishaa na wengine atawakomboa Ndugu,nachukia MTU anayetaka uongozi kwa kuharibu miradi ya MTU mwingine ,huyo afai kuwa kiongozi" amesema Mutabuzi
 Mmoja kati ya Wazazi aliyeongozana na Kijana wake katika usahili wa awamu ya kwanza.

 Katika picha ya pamoja na wanafunzi waliopokelewa chuoni hapo Jumapili ya leo
 Baadhi wa Vijana mara baada ya kuwasili Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Gera
Mnec Wilbroad pichani na Balozi Dr.Kamala mara baada ya kufanikisha utaratibu wa kuwakomboa Vijana Wilayani Missenyi  kwa kuanzisha  Mafunzo maalum ya kuwajengea uwezi waweze kujiajiri.



Next Post Previous Post
Bukobawadau