Bukobawadau

PUMZIKA MZEE FRANCIS B. BAYONA (1919-2021)

Mwendo umeumaliza, vita umevipiga. Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa Amani Mzee Francis Bayona (1919-2021) #letlovelead
Eng. Theodory Bayona ambaye ni mmoja kati  ya watoto wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Francis Bayona ,akiweka sawa Mwili ya mpendwa wetu muda mchache kabla ya utaratibu wa kutoa heshima za mwisho.
Mzee Frances Bayona amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 102,Mazishi yake yamefanyika siku ya Alhamis Jan 7,2021 Katika kijiji cha Kantare,Kata ya Bwanjai Parokia ya Mugana, Mazishi yake yameongozwa na Askofu Almachius Vincent Rweyongeza wa Jimbo katoliki Kayanga.
Mjukuu wa marehemu Mzee Frances Bayona,Branda Bayona akisoma Somo la Bwana wakati wa misa ya mazishi ya mpendwa wetu yaliyofanyika  Kijijini Kantare,Bwanjai Wilayani Missenyi
Waombolezaji wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Mzee  Francis Berchmans Bayona
Sehemu ya wanafamilia wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Mzee Francis Bayona
Mzee Francis Bayona alizaliwa 19,April 1919 Katika familia ya Mzee John Berchmans Kahwa Rugaze.

Marehemu Mzee Francis Bayona alipata elimu ya Msingi kwenye shule ya White Sisters,Mugana darasa la kwanza hadi la tatu kama ilivyokuwa kawaida kwa wakati huo.

Baada ya Shule hiyo Marehemu alikwenda Uganda,kufanya shughuli za Biashara.Mnamo mwala 1941 alirudi nyumbani na kufunga ndoa na Ma Geraldina Mukaite  tareheb 10/9/1941
Marehemu Mzee Francis Bayona enzi za uhai wake pichani kulia akiwa na Mtoto wake mkubwa Mzee Wincheslaus Bayona .

Mzee Francis Bayona  mwaka 1943-1945 alienda vita kuu ya pili  ya Dunia ambapo alipigana hadi nchini Kenya na ABYSSINIA ambayo ndiyo Ethiopoa ya sasa.

Wasifu wa Marehemu Mpendwa wetu Mzee Francis Bayona unasema; Baada ya Vita ya pili ya Dunia, ALIRUDI NYUMBANI Kijijini Kantare na mwaka 1949 alikwenda kupata elimu ya ufundi bomba Mgulani Jijini Dar es Salaam na kumalizia Ifunda Trainging School.
Wanakwaya wakiendelea kuwajibika kwa nyimbo za kumsifu Bwana
Taswira mbalimbali msibani hapo muda mchache kabla ya Ibada ya Mazishi ya Mpendwa wetu Mzee Francis Bayona ambaye alipata kufanya kazi katika kampuni ya David Burrow Dar es Salaam ambapo alikuwa incharge wa wa kitengo cha plumbing,Kampuni iliyokuwa ikifanya kazi za ujenzi na Serikali wakati huo.


Mwaka 1952 alirudi nyumbani na kufungua Duka la biashara jirani na Nyakijoga.Mwaka 1956-1975 alipata ajira Bukoba Town Council akiwa kama fundi bomba mkuu hadi alipostaafu mwaka 1975 na kurudi kijijini kuendelea na shughili za kilimo hadi mwisho wa maisha yake.

 Watoto;Mzee Francis Bayona alijaliwa kupata watoto 11,wakiume  saba (7) na wa kike wanne (4) walio hai mpala leo ni 9 wanaume sita (6) na wanawake watatu (3).

Marehemu Mzee Francis amejaliwa  wajukuu 52,Vitukuu 78 na Vilembwe 108.

Pichani ni sehemu ya wanafamilia ya Mpendwa wetu Mzee Francis Bayona aliyefariki na umri wa miaka 102.
Marehemu Mzee Francis alikuwa mtu wa  Ibada na hodari katika Imani ,alikuwa mwanachama wa shirika la Wafransico waliojulikana sana kama Watersial aliojiunga nao tangu mwaka 1950,Aliweza kushiriki Ibada za Misa siku zote hata katika uzee wake.

 Tumuombee pumziko la Amani Mzee wetu...!
Wanakwaya kama wanavyo onekana pichana...
Padre Tiba na Padre Karumuna wakiteta jambo...
Padre Deodatus Tiba akitolea jambo ufafanuzi wakati wa Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Mzee Francis Berchmans Bayona.

Baba Askofu
Almachius Vincent Rweyongeza wa Jimbo katoliki Kayanga akiongoza zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wetu.
Umati wa waombolezaji wakiwa wamejitokeza kwa wingi  katika Kitongoji cha Rugaze,Kijiji Kantare parokia ya Mugana kushiriki mazishi ya Mzee Francis Berchmans Bayona (102)

Padre Karumuna akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya wana Bwanjai waishio mikoani

Watoto wa Marehemu Mzee Francis Bayona wakiwa wameungana na wanafamilia wengine pamoja na waombolezaji katika Ibada ya Mazishi ya Mzee Francis Bayona

Mapadre wakitoa heshima za mwisho kwa Mzee wetu Mzee Francis Bayona ,Mzee aliyekuwa na karama ya uvumilivu na ustahimilivu maisha yake yote.

Padre Deodatus Tiba Paroko wa Parokia ya Mugana akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wetu Mzee Francis Bayona

Muendelezo wa matukio ya picha Marafiki wa marehemu wakitoa heshima zao za mwisho




Mzee Pontian Kashangaki Msemaji wa familia akisoma wasifu wa marehemu Mzee Francis Bayona na kutoa utambulisho kwa wanafamilia...


Mzee Wincheslaus Bayona ambaye ni mtoto wa kwanza wa marehemu Mzee Frances Bayona

Mzee Elizeus Bayona mwenye umri wa miaka 67 mmoja kati wa watoto wa kuzaliwa na Marehemu mzee Francis Bayona

Mtoto wa marehemu pichani wakati utambulishgo ukiwa unaendelea


Watoto wa Marehemu Mzee Francis wakati zoezi la utambulisho linaendelea..

Eng. Lambert Bayona wakati wa utambulisho

Utambulisho ukiendelea kwa watoto wa marehemu Mzee Francis Bayona


Ma Anatoria (82) ambaye ni Dada wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Francis Bayona




Mwongozaji wa shughuli nzima ya mazishi ya Mpendwa wetu.












Sister Joyce Imelda akiweka shada la maua...

Wanafamilia wakiendelea kuweka mashada kwenye kaburi la mpendwa wetu.


Prof Kaijage akiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa Mzee Francis Bayona (1919-2021)

Eng Theodory Bayona na mke wake wakiweka shada la maua

Bi Oliver Bayona akiweka Sawa shada la maua kwenye kaburi la mkwe wake.

Muendelezo wa matukio ya picha wakati utaratibu wa kuweka mashada ukiendelea..

Ndugu Bosco Bayona ambaye ni mjukuu wa marehemu mzee Francis Bayona akiweka shada la maua

Mtoto wa mwisho wa kiume kuzaliwa na Marehemu Mzee Francis Bayona,Eng Lambert Bayona na mke wake wakiweka shada la maua kwenye kaburi.

Baadhi ya wajukuu wakiweka shada la maua..
Padre Karumuna kama mwana ukoo akitoa neno..
Muendelezo wa matukio wakati wa kutoa salaam za rambirambi

Mh. Focas akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Bwanjai Community Group

Muendelezo wa matukio ya picha.

Salaam za rambirambi zikitolewa na Padre Anthony Lugundiza

Salaam za rambirambi zikendelea

Wawakilishi wa makundi mbalimbali wakiendelea kutoa salaam za rambirambi kifo cha Mpendwa mzee Francis Bayona



Vilio na machozi vikitawala kwa wanafamilia...

Simanzi ,vilio na machozi vikiendelea kutawala...

Hivi ndivyo hali ilivyokua katika Mazishi ya mpendwa wetu mzee Francis Bayona


 Tangulia Mzee wetu ,Vita umeipigana na mwendo umeumaliza.pumzika kwa amani Mzee Frances Bayona....
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiwa unaendelea...

Wakwe wa familia hii kwa pamoja wakitoa heshima zao za mwisho

Mzee Paschal B. Kabukoba ambaye ni mdogo wa marehemu Mzee Francis Bayona akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili ya mpendwa kaka yake.

Katikati ni mdogo wake Marehemu Mzee Francis B.Bayona,
Muendelezo wa matukio ya picha
Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Uncle Majid Kichwabuta pichani
Mzee Paschal B. Kabukoba akitoa heshima za mwisho.
Ma Anatoria ambaye ni Dada wa marehemu Mzee Francis Bayona akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa Kaka yake.

Eng Lambert Bayona akitoa heshima zake za mwisho

Eng Theodory Bayona wakati wa kutoa heshima za mwisho

Prof Kilama rafiki wa familia katika last respect kwa mpendwa wetu

Muendelezo wa matukio ya picha

Picha wakati wa kutoa heshima za mwisho

Umati wa waombolezaji katika mstari kumuaga mpendwa wetu Mzee Francis Bayona (102) 



Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu likiingizwa kaburini

Nenda Baba ,tangulia mzee wetu ,Vita umeipigana na mwendo umeumaliza ,Tutaonana Badae..

Lily,Brenda na Anna baadhi ya wajukuu wa Marehemu Mzee Francis Bayona wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Babu yao

Padre Karumuna akiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa wetu Mzee Francis Bayona
Padre Tiba   Baba paroko ya porokia ya mugana...

Taswira mara baada ya mazishi ya mzee wetu Mzee Francis Bayona

Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu.

Baadhi ya wajukuu katika picha ya kumbukumbu mara baada ya mazishi ya mpendwa mzee Francis Bayona

Wazee wakibadilishana mawazo mara baada ya mazishi ya mpendwa wetu Mzee Francis Bayona.
Familia inatumia furasa hii kutoa shukrani za dhati kwa masista wa  Kanosa (hawapo pichani) kwa huduma yao nzuri na madaktari waliojitahidi kuokoa maisha ya mzee wetu hususani wa hospitali ya Mugana

Katika hali ya simanzi anaonekana mdogo wa Marehemu Mzee Francis Bayona pichani kulia.

Kushoto pichani ni Mzee  Wincheslaus Bayona, mtoto mkubwa wa marehemu Mzee Francis Bayona, kwa sasa mzee huyu ana umri wa miaka 78.

Watawa wa kikatoliki wa Parokia ya Mugana ambao ni marafiki wa M pendwa wetu Mzee Francis Bayona wakiwa katika  picha ya pamoja na Mrs Oliver Bayona mara baada ya kumpumzisha mpendwa Mzee  Francis Bayona.
Uncle Majid Kichwabuta akiwafariji wafiwa pichani Eng na mke wake
Sehemu ya waombolezaji pichani kulia ni Mzee Yusuph Ngaiza

Muendelezo wa matukio ya picha Mazishi ya Mzee Francis Bayona
Awali Eng Theodory Bayona akijadiliana jambo na mapadre walioshiriki Ibada ya misa ya mpendwa Mzee wetu
Sehemu ya wanafamilia wakibadilishana mawazo
Bukobawadau tulipata fursa ya kufanya mahojiano na Mtoto mkubwa wa marehemu Mzee Francis Bayona,pichani ni Wincheslaus Bayona
Picha mbalimbali kutoka msibani hapa  Rugaze, Kantare Mugana katika Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu mzee Francis Bayona
#Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Kulia ni Mzee Egidius Bayona ambaye ni mtoto wa Marehemu Mzee Frances Bayona
Matukio ya picha za awali kabla ya Ibada ya mazishi....
Taswira eneo la maegesho...
Bukobawadau tunatoa pole kwa familia ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huu mkubwa,Daima Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele mzee wetu Mzee Francis Bayona.
Next Post Previous Post
Bukobawadau