Bukobawadau

UMATI WA WAOMBOLEZAJI WASHIRIKI MAZISHI YA VEDASTINA TEOPHIL -BIIRABO MULEBA

Muonekano wa Jeneza lenye Mwili wa Mpendwa wetu Vedastina Teophil (1935-2020)
R.I.P Mama yetu mpendwa Ma Vedasina Teophil,Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi,Umekua msaada kwa wengi,pengo lako ni kubwa mnoo Mama,Inauma sana,lala Salama ,tutaonana badae Mama.
Wachungaji wakiongozwa na Mchungaji  Essau Bililiza katika Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Vedastina Teophil yaliyofanyika Jan 1,2021 Kijijini  Ruhanga- Bilambo Wilayani Muleba
Mzee Cathbert Basibila miongoni mwa waombolezaji walishiriki Mazishi ya mpendwa wetu Ma Vedastina Teophil yaliyofanyika nyumbani kwake  Kijijini Ruhanga -Bilabo Wilayani Muleba.
Kwa ufupi historia ya Mtwaliwa mpendwa wetu Ma Vedestins Bwankazi Teophil aliyezaliwa tarehe 1.7.1935 Katiks kitongoji cha Katembe kata ya Biirabo Wilaya ya Muleba akiwa mtoto wa kwa kuzaliwa kwa familia ya Ta Obadia Rwayumbs na Mama yake Ma Nshoro.
ELIMU;Mwaka 1945,aliandikishwa shule ya Msingi Nyakasambi-  Biirabo wakati huo shule ikiitwa Bush School ambapo alisoma na kihitimu darassa la Nne mwaka 1950.
Mnano Mwaka 1945 Mpendwa wetu Ma Vedastina aliolewa na Mzazi wetu Marehemu Ta Teophil Muhoza Rwakalaza Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponita,Nab kwa pamoja walijaliwa kupata watoto tisa,Sita wakiwa Wakike na watatu wa kiume,Kati yao Watato watato watano walikwisha tangulia mbele ya haki.
Mpaka hivi leo watoto  wa mpendwa Ma Vedastina walio hai ni watoto wa nne na mtoto wa Mwisho kutwaliwa kabla ya Mama ni Kaka mkubwa wa familia Edward aliyeaga Dunia mapema tarehe 2.12.2020 yaani mwezi mmoja uliopita......'Tumuombee pumziko la Amani Kaka yetu'
Taswira  mbalimbali katika picha Mazishi ya Mpendwa Ma Vedastina Teophili aliyefikwa na umauti tarehe 29.12.2020 siku ya jumanne majira ya saa 9:30 Alasiri
Familia inatumia fursa hii ku kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumleta Mama yao Duniani na kumjalia uhai wa miaka (85) miezi  mitano na siku (29) na kumchukua kwa tarehe, muda na wakati aliochagua yeye muumba......!
Familia inamkumbuka mpendwa Mama yao kwa mengi,Machache kati yake yaki ni 'UPENDO' Usiopimika kwa wanae,kwa familia yake,ndugu zake na majirani kwa ujumla wao...
Marehemu Ma Vedastina Teophil alikuwa 'Mkweli' ,Mcha Mungu na Mchapakazi aliyethamini na kuwafundisha wanae kuridhika na matunda ya mikono yao.
Mpendwa wetu Ma Vedastina  Bwankazi Teophil alimpenda Mungu wake,Kwani kila siku jioni baada ya chakula yeye pamoja na Wajukuu wake walisoma Neno la Mungu kutoka kitabu cha Biblia Takatifu Siku zote uimba na kusali kabla ya kupanda kitandani
Mmoja kati ya watoto wa kuzaliwa na Mpendwa Ma  Vedastina Teophil
Lameck Rwakalaza mmoja kati ya watoto wa kuzaliwa na Marehemu Vedastina Teophil akishiriki Ibada ya mazishi ya mpendwa mama yetu....
Mchungaji wa Anglina akiongoza mazishi ya Mama yetu Mpendwa Ma Vedastina Teophili...
Mpendwa Ma Vedastina Teophil ameacha Watoto Wanne (4) ,Wajukuu ishirini na mbili (22) Vitukuu (40) na Vilembwe vinne (4)
Kijana Amon Frela pichani katikati akishiriki Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Ma Vedastina Teophil



Muongozaji wa shughuli ya Mazishi hayo Mc Rutajula Kandaga akitolea jambo ufafafanuzi kwa mujibu wa ratiba.





Wasifu wa Marehemu ukisomwa na  Adv Benard Buberwa Buhoma mtoto mkubwa wa mapendwa wetu Ma Vedastina Teophil.

Sehemu ya watoto wa kuzaliwa na mpendwa wetu Ma Vedasina Teophil

Bi Purakseda Rwakazaji akitoa neno  na shukrani kwa niaba ya familia

Bi Purakseda Rwakazaji akitoa neno  na shukrani kwa niaba ya familia..

Familia ya Adv.Kamala wa Ishozi wakitoa Salaam za rambirambi
Familia ya Barongo wa Inshunju -Kiziba kwa pamoja wakati wa kutoa salaam za rambirambi.
Sehemu ya wakwe wa familia kutoka Jijini Mwanza wakifuatilia kinachojiri
Mkono wa pole kwa Adv Bernard Buberwa Buhoma kutoka kwa wanafamilia ya Balongo wa Inshunju
Wanafunzi waliosoma Shule ya Msingi Birambo wakikabidhi ubani wao kwa wafiwa..
Mchungaji Samson Paul,Mchungaji mstaafu wa KKKT akitoa neno kufuatia kifo hiki cha mpendwa Vedastina Teophil
Ndugu Byamungu akiwa ameungana na waombolezaji wengine
Muendelezo wa matukio utaratibu wa salaam za rambirambi ukiwa unaendelea..
Wanafamilia nao kwa umuhimu wakitoa rambirambi na zawadi kwa wale wote walioshiriki kumuuguza mpendwa wetu Ma Vrdastina Teophil
Taswira mbalimbali eneo la msibani hapa waombolezaji wakiwa wameungana na wanafamilia...
Kimila zaidi Bwana Cathbert Baibila akisalimia na  wafiwa mara baada ya kukabidhi     Sanda 'Ekilago' kwa Kaka Bernard Buhoma
Makundi mbalimbali yakiendelea kutoa rambirambi kwa wanafamilia


Endelea kufuatilia kurasa zetu za facebook  kwa matukio zaidi ya picha

Umati mkubwa wa waombolezaji wameshiriki mazishi ya Mpendwa Vedastina Teophil .
Umati wa waombolezaji mazishi ya Ma Vedastina Teophil  Kijijini Ruhanga Birabo-Muleba
Muendelezo wa matukio ya picha
Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Salaam za rambirambi kutoka kwa Uongozi wa Serikali ya Kijiji
Utaratibu wa kukabidhi rambirambi ukiwa unaendelea
Muda mchache kabla ya kuelekea eneo la kaburi

Jeneza lenye Mwili wa mpendwa Mama yetu Vedastina Teophil likiwa limebebwa... kuelekea eneo la kaburi
Mchungazi akingoza utaratibu wa kuweka  udongo kwenye kaburi
Mpendwa Ma Vedastina Teophil ameacha Watoto Wanne (4) ,Wajukuu ishirini na mbili (22) Vitukuu (40) na Vilembwe vinne (4) 'Nenda Mama... tangulia Mama tutaonana badae..'
Watoto wa Marehemu Ma Vedastina Teophil awakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao mpendwa...
Adv.Kamala na mke wake wakiweka Shada la maua kwenye kaburi la mpendwa Vedastina Teophil
Marafiki wa familia wakiendelea kuweka mashada ya maua..
Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sehemu ya Wajukuu wa mpendwa wetu Ma Vedastina wakiweka Shada la maua
Wajukuu wakendelea na utaratibu wa kuweka mashada ya maua
Taswira mbalimbali eneo la kaburi utaratibu wa kuweka mashada ukiwa unaendelea
Mama Wawili mkwe wa familia akiweka mashada sawasawa
Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Muendelezo wa matukio ya picha mara baada ya mazishi
Pole Sana Mkurugenzi wa Gateway Rodge Arusha,Adv Benard Buhoma

Mwisho,Burudani ya ngoma kutoka kwa Wajukuu ikiendelea kuchukua kasi...

 


Next Post Previous Post
Bukobawadau