Bukobawadau

KASHAMBYA HOSPITAL ILIYOPO GERA YAZINDULIWA RASMI

Kituo Cha Afya Cha Kashambya kata Gera wilayani Missenyi mkoani Kagera ambacho kitatoa huduma za kitabibu kwa magonjwa mbalimbali ya binadamu kimefunguliwa ,ikiwa ni sehemu ya kutimia kwa ndoto ya Dr Consolata Banda Rwechungura mkazi /Mzaliwa wa kata Gera ambaye amekuwa ajitolea katika jamii ya Gera kwa zaidi ya miaka 20 kwa kuleta madaktari Bingwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutoa huduma za Afya kwa wananchi.
Ufunguzi wa kituo hicho Cha Afya umewashirikisha viongozi wa serikali Ngazi ya Afya wa wilaya na mkoa pamoja na Askofu wa Jimbo la Kayanga Almachius Rweyengoza Ambaye aliwataka wananchi wanaoishi nje ya nchi kukumbuka Nyumbani na kuja kuwekeza vitu vitakavyoisaidia jamii na kuacha alama kumbukumbu katika Maisha ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
Ukamililaji wa kituo hicho kitakachotoa huduma zote za kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya Binadam ni ndoto ya Dr Consolata Rwechungura ambayo aliishi nayo kwa kipindi Cha Miaka 20 iliyopita ambapo alilazimika Kuwaleta madaktari Bingwa kutoka Marekani na kuja kuwatibu magonjwa mbalimbali wakazi wa mkoani Kagera bila kuwa na eneo la kutosha la kutolea huduma za Afya zoezi hilo la kuleta madaktari limekuwa likifanyika kila baada ya miaka 2.
Hata hivyo wananchi wa Kata Gera wakiongozwa na Diwani wa kata hiyo Mh Bitegeko (pichani kulia) waliosimama wamepongeza hatua hiyo na kusema kuwa hata wangeandika kitabu kuhusu mazuri yaliyofanywa na Dr Consolatha huenda wangekesha wakiandika kwa sababu ndani ya miaka 20 amejenga shule,amesomesha watoto,ametoa huduma za tiba,ametibu wazee ,ameleta maji,ametengeneza mifumo ya umeme shuleni ,amefadhili miradi ya jamii na mengine mengi ambayo yanaitimishwa na uwepo wa kituo hicho katika Kijiji Chao ambacho kitawapunguzia mwendo wa kufata huduma za Afya katika hospital zilizoko mbali.
Katika picha ya pamoja 
na Askofu Almachius Rweyongeza wa
Jimbo Katoliki la Kayanga mara baada ya  misa takatifu ya kumshukuru Mungu na kubariki Majengo ya mradi wa Hospital ya Kashambya iliyopo Kata Gera Wilayani Missenyi
Viongozi wa Kiserikali wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RMO) Isandela Kaniki waliosimama pichani katikati pamoja na wadau na wauguzi  wa Kashambya Hospital
Muendelezo wa matukio ya picha kwa ajili ya kumbukumbu na Dr Consolatha Banda Rwechungura.
Wazee wa Kata ya Gera  na Uongozi wa Kashambya Hospital katika picha ya pamoja mara baada ya Baba Askofu Almachius
Rweyongeza kubariki majengo ya Hospital hiyo.
Muonekano wa Majengo ya Hospital ya Kashambya kwa Nje.
Chumba cha Daktari
Taswira ndani na nje ya Majengo kupitia Bukobawadau
Dr  Consolatha Banda Rwechungura pichani (MD) Kashambaya Hospital
Tumeshuhudia Sehemu ya Vifaa tiba katika  Hospitali hiyo Kashambya  ikiwemo mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti,mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali
Vifaa tiba vya aina mbalimbali
Ndani ya vyumba wataalam wa Afya na Wagonjwa
Vifaa mbambali ndani ya Hospital hiyo....
Muonekano wa Sehemu mbalimbali za Majengo ya Hospitali ya Kashambya
Generator lenye uwezo wakutoa umeme kulingana na mahitaji
Jengo la Jiko hospitali ya Kashambya.
Wadi za Wagonjwa kama inavyo onekana pichani
Vyoo ndani ya hospitali ya Kashambya -Gera Missenyi
Wananchi wa Kata Gera wakiongozwa na Diwani wao Mh.Bitegeko wameonyesha furaha yao  huku wakimuombea Mwenyezi Mungu amlinde Dr.Consolatha Banda Rwechungura
Taswira mbalimbali pichani Hospitali ya Kashambya
Ndani ya Chumba cha Uzazi (Labor)......

Muendelezo wa matukio ya picha...
Mganga mkuu Dr Samson William wa Hospital ya kashambay akitolea jambo ufafanuzi wakati wa Ukaguzi wa Majengo ya Hospitali hiyo
Dr.Consolatha Banda akitolea jambo ufafanuzi ndani ya chumba cha Uzazi
Sehemu ya Mapumziko kwa Wauguzi na Madaktari wa hospitali ya Kashambya
Kuelekea chumba cha Mapumziko kwa Wauguzi na Madaktari wa hospitali ya Kashambya
Vyumba vya Private hospitali ya Kashambya iliyopo Gera Wilayani Missenyi

Muonekano wa picha ya Juu Baadhi ya Majengo ya Hospitali ya Kashambya

Sehemu ya maegesho ya magari.
Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote pale wasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Pia tuna Offer kabambe ya coverage ya Picha na video kwenye sherehe mbalimbali hii ni Huduma kutoka kwetu Siku zote @bukobawadau

Muonekano wa picha ya Juu Baadhi ya Majengo ya Hospitali ya Kashambya..

INTRO SEHEMU YA VIDEO   UZINDUZI NA MISA YA SHUKRANI HOSPITALI YA KASHAMBYA GERA

Next Post Previous Post
Bukobawadau