Bukobawadau

MH.WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA:MGENI RASMI BARAZA LA MAULID KAGERA LEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kwenye Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera leo .

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye Baraza la Maulidi Kitaifa, lililofanyika Kitaifa katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ally akizungumza na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kwenye Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Umati wa Waumini wakimsikiliza S
heikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir
Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir amesisitiza haja ya waumini wa madhehebu mbalimbali za dini hapa nchini kushikamana zaidi.

Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba,Askofu Methodius Kilaini na amejumuhika  na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Burudani ikiendelea
katika Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Sheikh
Abdul Rafiu akifurahi  nyimbo za kumtukuza Mtume Muhammad  katika Baraza la Maulidi Kitaifa, lililofanyika Kitaifa katika viwanja vya Kaitaba, Mjini Bukoba, mkoani Kagera leo
Bwana Hamza Itembwe,Mwalimu Amini na Kaka Athman miongoni mwa wanakamati ya Miundombinu
Maulidi ya kuadhimisha Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) kitaifa yaliofanyika katika viwanja vya Kaitaba Mjini Bukoba leo.

Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Kiislamu ya Bakwata, Hajaat Shamimu Khan akifatilia kinachojiri katika Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Mwenyekiti wa ccm Mkoa Kagera Mama Buhiye wakati wa Utambulisho
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeonesha kwa vitendo kuongoza Taifa na kufikisha maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali tofauti za kidini na ukabila.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kusimamia mshikamano, haki na umoja wa Taifa, hivyo amewasihi Watanzania wote waendelee kumuombea Rais Samia ili aendelee kuiongoza vyema nchi yetu.
Ameyasema hayo leo Jumanne (Oktoba 19, 2021) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia katika Baraza la Maulid lililofanyika Kitaifa katika uwanja vya Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera.
Waziri Mkuu amewataka waumini wa dini ya Kiislam nchini watumie maadhimisho hayo kama fursa muhimu kwao kuyasoma na kuyatafsiri kivitendo maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W) katika mfumo wao wa maisha ya kila siku.
“ Tafakuri hiyo ituwezeshe kuishi maisha ya undugu, kupendana, kuheshimiana na kushikamana miongoni mwetu Waislam pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.”
Akizungumzia suala la amani na utulivu Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa amani ni tunu adhimu ambayo Mwenyezi Mungu ametukirimia kwani kuishi kwa amani ni kumfanya ibada Mwenyezi Mungu.
“Kudumisha amani iwe ni wajibu wa kila mmoja wetu kwani amani ndiyo kila kitu. Bila amani hatuwezi kupata maendeleo, hatuwezi kufanya ibada, watoto wetu hawawezi kwenda shule na mambo mengine mengi”

Ameongeza kuwa Tanzania imekuwa kinara katika kuenzi na kudumisha amani, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuendelea kuitunza amani hiyo kwa kuwafundisha vijana na watoto misingi ya amani ili nao waidumishe.
“Serikali inatambua umuhimu wa madhehebu ya dini katika kudumisha amani. Viongozi wa dini mmekuwa mabalozi wema na kudumisha amani yetu kwa miongo kadhaa. Jitihada zenu zote zimewezesha nchi yetu kupata utulivu kila wakati na aghalabu kuwa kimbilio la majirani pindi wanapopata machafuko.”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasihi viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kufanya maandalizi kwa ajili ya kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti mwakani.
“Zoezi hili litaiwezesha nchi kupata takwimu za msingi zinazotumika katika kutunga sera, kupanga mipango na programu za maendeleo pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.”
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanja chanjo ya kujikinga na UVIKO 19. “Suala la afya ni muhimu na si la kufanyia maskhara.Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Samia ameshazindua kampeni ya chanjo dhidi ya UVIKO 19. Tumuunge mkono.”
Kwa upande wake, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally amewasihi wananchi waendelee kuwaheshimu na kuwatii viongozi wao wa dini na Serikali kwa sababu hiyo ndiyo tabia njema ambayo inachangia Taifa kuwa na maendeleo.
Naye, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Nuhu Jabir ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia kwa namna inavyowahudumia wananchi kwa kutoa takribani trilioni moja kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeo.

Muendelezo wa matukio ya picha Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Hajjath Mwajabu  Galiatano na Mama Byabato pichani
Picha katika Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Muendelezo wa matukio ya picha
Ndugu Ashraf Kyobya  pichani
Taswira mbalimbali katika Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
Alhaj Suleiman Kova (mjumbe wa bodi ya wadhamini) Bakwata Taifa.

Bi Sophia Hamad pichani
Picha mbalimbali katika Baraza la Maulidi lililfanyika katika viwanja vya Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera. Oktoba 19, 2021
 

Next Post Previous Post
Bukobawadau