Bukobawadau

ALPHONCE FELIX SIMBU ASHINDA MEDALI YA FEDHA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA JIJINI BIRMINGHAM UINGEREZA LEO


Mwanariadha Alphonce Felix Simbu akiwa na furaha kwa kutwaa medali ya Fedha baada ya kuibuka mshindi wa pili mbio za marathon katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza, nyuma ya Victor Kiplagat wa Uganda. Pamoja naye ni mkimbiaji Hamisi Misai ambaye alimaliza katika kumi bora ya mashindano kwa kushika nafasi ya nane.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na timu ya Taifa ya Riadha pamoja na mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya kushinda medali ya Fedha kwa kuibuka mshindi wa pili mbio za marathon katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza, nyuma ya Victor Kiplagat wa Uganda leo. Mkimbiaji Hamisi Misai  (wa tatu kulia) alimaliza katika kumi bora ya mashindano hayo kwa kushika nafasi ya nane. Wa pili kutoka kushoto ni Failuna Matanga ambaye alimaliza mtu wa tano katika marathon ya wanawake wakati Jackline Sakilu (wa pili kulia) akimaliza mwishoni akichechemea kutokana na maumivu ya msuli aliyoyapata akiwa kilomita 17 tu ya mchuano huo. Hivyo alichechemea hadi akamaliza huku akishangiliwa sana na umati mkubwa wa watu uliokuwepo. Kushoto ni kocha mkuu Suleiman Nyambui na kulia ni kocha msaidizi Lwiza John

Mwanariadha hodari Failuna Matanga akipongezwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro na Watanzania wengine kwa kumaliza wa Tano katika mbio za Marathon kwa wanawake kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza leo.


Mwanariadha hodari Failuna Matanga akipongezwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro na Watanzania wengine kwa kumaliza wa Tano katika mbio za Marathon kwa wanawake kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza leo.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania na Baraza la Michezo wakifuatilia katika runinga kubwa jinsi mwanariadha Alphonce Felix Simbu akipambana na  kushinda medali ya Fedha kwa kuibuka mshindi wa pili mbio za marathon katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza, nyuma ya Victor Kiplagat wa Uganda leo. 


Walishudia pia mkimbiaji Hamisi Misai akimaliza mbio katika kumi bora ya mashindano hayo kwa kushika nafasi ya nane, huku kwa wanawake Failuna Matanga alimaliza mtu wa tano wakati Jackline Sakilu akimaliza mwishoni huku akichechemea kutokana na maumivu ya msuli wa paja aliyoyapata akiwa kilomita 17 tu ya mchuano huo. Hivyo alichechemea hadi akamaliza huku akishangiliwa sana na umati mkubwa wa watu uliokuwepo.


 




 

Next Post Previous Post
Bukobawadau