Bukobawadau

WANANCHI MWALO WA IGABIRO BUKOBA WAPATIWA ELIMU NA HAMASA KUHUSU KAMPENI YA CHANJO YA POLIO

Timu ya Wizara ya Afya imefika katika Mwalo wa Igabiro uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kutoa Elimu na Uhamasishaji kuhusu Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8.

Beauty Mwambebule Mtaalam kutoka Wizara ya Afya amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapatiwa Chanjo ya Polio pindi kampeni ya utoaji wa Chanjo itakapoanza tarehe 21 hadi 24, Septemba 2023 na kutoa ushirikiano kwa watoa huduma watakao watembelea nyumba kwa nyumba kutoa Chanjo hiyo.

Aidha Beauty ameongeza kuwa wazazi ambao hawatokuwepo majumbani kipindi Kampeni waweze kushirikiana na majirani zao pindi watakapokuwa wametoka majirani waweze kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha watoto wanapatiwa Chanjo pindi watoa huduma watakapopita ili kuikinga jamii nzima.

Aidha katika Kampeni hiyo watoa huduma au timu za wachanjaji watapita  nyumba Kwa nyumba, shuleni, sokoni na sehemu zingine zenye mikusanyiko ili kuhakikisha kila mtoto anapata Chanjo hiyo.

Naye Bw. Chambu Ngeleja katibu wa BMU (Beach Management Unit) ameishukuru Timu ya Wizara ya Afya kuwatembelea na kutoa elimu na kuhamasisha jamii watoto kuweza kupata Chanjo ya Polio, amesisitiza uhamasishaji huo utaendelea katika eneo hilo la Mwalo na kuhakikisha kila mtoto anapata Chanjo ya Polio ili kuwakinga watoto hao

 

Next Post Previous Post
Bukobawadau